Tarehe 13 Juni 2024
Tangu tuliporejesha Kupiga simu kwenye WhatsApp mwaka wa 2015, tumeendelea kuiboresha kwa kuanzisha simu za vikundi, simu za video na usaidizi wa mifumo mingi.
Leo tuna masasisho kadhaa yatakayofanya kupiga simu kwenye vifaa vyako kuwa mazuri na bora zaidi, yatakayoanza kutumika katika wiki chache zijazo:
Pia tunaangazia ubora wa sauti na video bila kuchoka, kwa simu nzuri zaidi bila kujali mahali ulipo. Hivi majuzi tulizindua kodeki ya MLow ambayo inaboresha utegemezi wa simu. Simu zinazopigwa kwenye vifaa vya mkononi hunufaika kutokana na kughairiwa kwa kelele na mwangwi kulikoboreshwa, hivyo kurahisisha kupiga simu katika mazingira yenye kelele, na simu za video huwa na ubora wa juu kwa wale walio na miunganisho ya haraka zaidi. Sauti ni shwari kwa ujumla, hata kama una muunganisho duni wa mtandao au unatumia kifaa cha zamani. Unaweza kusoma zaidi kuhusu kodeki ya MLow na kusikiliza tofauti katika ubora wa sautihapa.
Tutaendelea kufanya maboresho ya kupiga simu kwenye WhatsApp ili uweze kupiga simu za faragha za ubora zaidi popote ulipo duniani.